Azam - Local

Azam Fc tayari kuanza maandalizi ya 2024/25

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Jun 2024
Azam Fc tayari kuanza maandalizi ya 2024/25

Azam FC imetangaza kuanza kurejea kambini Julai Mosi hadi nne rasmi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25

Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu hiyo Thabit Zakaria (Zakazakazi) amesema timu hiyo itaanza kupokea wachezaji kuanzia Julai Mosi hadi nne ambapo rasmi kikosi hicho kitafanya mazoezi Julai tano hadi sita kwenye Uwanja wa Azam Complex

Ameongeza kuwa kikosi hicho kitasafiri kwenda Zanzibar kwa kambi ya siku sita kuanzia Julai sita hadi 13 ambapo kitarudi Dar es Salaam 

Julai 14 kikosi kitaelekea Morocco kwenye kambi ndefu hadi mwishoni mwa mwezi

Zaka amesema tayari kikosi hicho kimeshaachana na wachezaji wake watano ambao ni Issah Ndala, Malckou Ndoye, Edward Manyama, Daniel Amoah na Ayoub Lyanga lakini sio mwisho kwani lolote linaweza kutokea katika dirisha hili la usajili

Ameongeza kuwa kikosi hicho kwenye msimu wa 2024/25, kitajikita zaidi kwenye kuwania ubingwa kwenye mashindano watakayoshikiri kwani kutwaa ubingwa ndio itakuwa furaha yao

Azam FC msimu ujao itashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu, FA, Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi. Hadi sasa Azam FC imetambulisha wachezaji watano wanne wa nje na mmoja wa ndani.

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
3m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
32m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’