Klabu ya Simba imemuongeza mkataba wa miaka miwili kiungo asiyechoka Mzamiru Yassin
Baada ya kuonyesha kiwango bora katika msimu uliopita, uongozi wa Simba umejiridhisha kuwa Mzamiru anastahili kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi
Mzamiru ni miongoni mwa wachezaji waandamizi waliobaki katika kikosi cha Simba
Ameitumikia Simba kwa misimu nane, mkataba wake mpya utamfanya adumu Msimbazi mpaka mwaka 2026