Mapema wiki hii Yanga ilithibitisha kuachana na mlinzi wa kushoto Joyce Lomalisa baada ya mkataba wake kumalizika
Yanga tayari imemshusha nchini mlinzi wa kushoto Chardack Boka nae kutoka DR Congo
Boka (24) alikuwa akiitumikia klabu ya FC Lupopo ya huko DR Congo, ndiye anayetarajiwa kurithi mikoba ya Lomalisa
Wakati Yanga ikitarajiwa kuanza maandalizi ya pre-season Avic Town hapo kesho, ni suala la muda kwa Boka na nyota wengine wapya waliosajiliwa kutambulishwa
Mpaka sasa Yanga imetambulisha wachezaji wawili wapya, Clatous Chama na Prince Dube
Taarifa za ndani ni kuwa bado kuna 'vyuma' vingine vitatu vinasubiri utambulisho



