Klabu ya Simba imetangaza kuachana na mshambuliaji Pa Omary Jobe ikiwa miezi sita tu tangu alipojiunga na Wekundu hao wa Msimbazi
Taarifa iliyotolewa na Simba mapema leo, imebainisha kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya nakubaliana ya pande mbili
Katika kipindi alichoitumikia Simba, Jobe alishindwa kuonyesha makali yake akifunga bao moja pekee
Lilikuwa ni suala la muda tu Jobe kupewa mkono wa kwaheri kwani aliachwa jijini Dar es salaam wakati wachezaji wengine wakisafiri Misri kwa ajili ya pre-season



