Azam Fc yamnasa Diakite

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th July 2024


Azam Fc yamnasa Diakite

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Mali, Cheickna Diakite, kutoka klau ya Real Bamako

Nyota huyo chipukizi, 19, aliyepachikwa jina la staa wa Real Madrid Mbappe, kutokana na kasi na uwezo wake wa kuipenya safu ya ulinzi ya timu pinzani, amesaini mkataba wa miaka mitatu utakaomfanya kudumu ndani viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2027

Diakite ametua Azam Fc kuchukua nafasi ya Kipre Junior ambaye ametimkia klabu ya MC Algiers

Azam Fc tayari wamethibitisha usajili wa winga huyo ambaye amewahi kuhusishwa na vigogo wa soka nchini klabu za Yanga na Simba


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.