Yanga yaomba muda mapitio ya kesi

Joel JJ By Joel JJ β€’ 17th July 2024


Yanga yaomba muda mapitio ya kesi

Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick amesema tayari klabu imechukua hatua kwa kuomba muda zaidi wa mapitio kwa kuwa hawakushirikishwa katika kesi iliyoamuliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es salaam

Aidha Simon amesema Yanga itachukua hatua dhidi ya wahusika walifungua kesi hiyo na hatua zaidi zitachukuliwa na Wanachama wa Yanga kupitia Mkutano Mkuu

Simon amesema uongozi wa Yanga utaendelea na majukumu yake kwa kuwa walioshitakiwa ni Baraza la Wadhamini

"Tumegundua kuna kundi la watu linalowatumia hawa watu kuvuruga amani na tayari klabu kushirikiana na Vyombo vya Usalama tumeanza kuwafanyia uchunguzi hawa watu ambao wako nyuma yao"

"Ikibainika wote watapelekwa mbele ya mkutano Mkuu kama ni wanawachama mkutano mkuu utachukua hatua"

"Kesi walifungua mwaka 2022 kabla ya uongozi wetu haujaingia madarakani. Mei 2024 walalamikaji walipeleka maombi ya kukazia hukumu kwa Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba Mahakama kulifuta baraza la wadhamini wa Yanga na kuutoa uongozi wa Yanga na kutaka wakabidhiwe timu na Asset zote za Yanga waendeshe wao"

"Baada ya kufanya hivyo Juni 10, 2024 klabu ilipata taarifa kwamba kuna kundi la watu wamepeleka maombi Mahakamani kuomba uongozi wa Yanga uondolewe na wakabidhiwe klabu hiyo"

"Uongozi wa Yanga chini ya Rais Eng. Hersi na Jopo la Mawakili tulianza kufuatilia suala hilo na kugundua kuwa, kesi hiyo iliendeshwa kwa upande mmoja kwa hawa watu kugawana majukumu kwa upande wa mlalamikaji na mlalamikiwa"

"Tuligundua Juma Ally Abeid aligushi sahihi ya Klabu na kujifanya Mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa klabu, aligushi sahihi ya Mama Fatma Karume akijidai mwakilishi wake, aligushi sahihi la Mzee wetu Jabil Katundu ambaye alilazimishwa kuingia kwenye hili shauri" 

"Kutokana na kutoitambua katiba ya 2010, wanadai wanachama wote si halali, hivyo na Viongozi wote na uanachama wao ambao wanauita wa Katiba ya 2010 ni batili, kwa maana Rais wa Klabu, Makamu wake, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Viongozi wote walioajiriwa kwa kigezo cha uanachama ni batili pamoja na kazi zote zilizofanywa na Viongozi wote waliopo madarakani nazo ni batili na wanataka ripoti ya fedha na matumizi wakabidhiwe," alisema Simon


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.