Singida - Local

Kitambi aahidi makubwa Singida BS

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Jul 2024
Kitambi aahidi makubwa Singida BS

Kocha Msaidizi wa klabu ya Singida Black Stars, Denis Kitambi, amesema usajili walioufanya na uwepo wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems anaamini timu hiyo itacheza michuano ya kimataifa msimu ujao

Akizungumza kutoka mkoani Arusha ambako timu hiyo imeweka kambi yake kujiandaa na msimu ujao, Kitambi alisema malengo yao msimu ujao ni kuhakikisha timu hiyo inapata nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa

"Kwa wachezaji waliopo ndani ya timu hii tuna matumaini makubwa ya kushiriki mashindano ya Kimataifa msimu ujao mashabiki wategemee burudani kutoka kwetu, uwepo wa wachezaji wenye uwezo na benchi zuri la ufundi itatufikisha pale tunapotaka kufika," alisema Kitambi

Aidha, alisema wachezaji wao wana viwango vya cha Kimataifa ambavyo vitaleta ushindani mkubwa msimu huo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.

Alisema tangu ajiunge na timu hiyo wachezaji na viongozi wamempa ushirikiano mkubwa hali inayompa matumaini ya kutimiza malengo yao

Kwa upande wake Ofisa Habari wa timu hiyo, Hussein Masanza akizungumzia hali ya kambi yao alisema kila kitu kinaenda vizuri huku morali yavwachezaji ikiwa juu. Amewahaidi mashabiki kupata furaha kutokana na aina ya wachezaji waliowasajili msimu huu.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’