Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Julai 22 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Jul 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Julai 22 2024

Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano ya thamani ya pauni milioni 42.1 na Bologna kwa beki wa Italia Riccardo Calafiori, 22. (Sky Sports)

West Ham wana nia ya kutaka kumnunua beki wa AC Milan mwenye umri wa miaka 26 Muingereza Fikayo Tomori. (Mail)

Aston Villa wako tayari kumuuza beki wa kulia wa Poland Matty Cash mwenye umri wa miaka 26 msimu huu mpya. (Football Insider)

Manchester United wameamua kutoanzisha chaguo la kumsajili kiungo wa kati wa Morroco Sofyan Amrabat, 27, kwa mkataba wa kudumu. (Tuttomercato - In Itali)

Klabu hiyo ya Ligi ya Premia ina nia ya kumbakisha Amrabat katika klabu hiyo baada ya muda wake wa mkopo msimu uliopita lakini wanataka kufanya mazungumzo ya mkataba mpya. (Metro)

Mshambuliaji wa Aston Villa Mfaransa Moussa Diaby, 25, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Al Ittihad wiki ijayo. (Sportsport)

Villa watatafuta kuchukua nafasi ya Diaby na kumchukua mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix, 24. (Sun) Tottenham wanataka kumbadilisha Oliver Skipp na kiungo wa nyumbani ikiwa watamruhusu Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 23 kuondoka katika klabu hiyo. (Football Insider)

Rais wa heshima wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness amependekeza beki Mholanzi Matthijs De Ligt, 24, ambaye anasakwa na Manchester United, akuondoka katika klabu hiyo msimu huu . (Sky Germany)

Kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, hajaafikiana makubaliano na klabu ya Saudi Arabia Al Ittihad licha ya kuwepo kwa ripoti. (Sportsport)

United hawataki kumruhusu kiungo wa Scotland Scott McTominay, 27, kuondoka Old Trafford, hukuFulham na Tottenham zikimnyatia. (Standard)

Paris St-Germain wako tayari kuendeleza harakati zao za kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25. (Fabrizio Romano)

Pamoja na Osimhen, PSG pia wanataka kuwasajili winga wa Napoli wa Georgia Khvicha Kvaratshkelia, 23, na kiungo wa kati wa Ufaransa Desire Doue mwenye umri wa miaka 19 kutoka Rennes. (Sky Sports)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’