Wiki ya Simba kuzinduliwa Mikumi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Jul 2024
Wiki ya Simba kuzinduliwa Mikumi

Klabu ya Simba leo imetangaza kuzinduliwa kwa shamrashamra kuelekea Simba Day ambayo kilele chake ni August 03 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Simba imepanga kuzindua wiki ya Simba mkoani Morogoro ambapo Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Imani Kajula amesema uzinduzi huo utafanyika katika mbuga ya Mikumi

Kajula amesema kuna matukio mengi yameandaliwa katika uzinduzi huo ambapo amewataka Wanamsimbazi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu

"Tunalenga kuzindua Simba Week ndani ya mkoa wa Morogoro ndani ya Hifadhi ya Mikumi. Simba ni timu ya watu wote ndio maana tumewapa heshima Wanasimba wa Morogoro kufanya uzinduzi na kitovu itakuwa Mikumi tukianza safari kwa muda wa saa 1."

"Kwenye mbuga ya Mikumi sio tu kufanya uzinduzi na kurudi, kuna uwanja mzuri sana wa mpira na Ahmed atazungusha namba 6, yawezekana pia Ally Kiba akawepo. Mimi nitazungusha namba 10. Ubaya Ubwela hadi kwenye mbuga za wanyama," alitamba Kajula

"Wiki ya Simba itakuwa na mambo mengi kama kusaidia jamii, kuamsha hamasa ya mashabiki, kuenzi waasisi wa Simba lakini pia michezo ni sehemu ya utalii ndio maana mara nyingi sana Simba tumekuwa tukioanisha mikakati yetu na ya utalii"

Aidha TRC kupitia treni ya mwendo kasi watasafirisha mashaiki kutoka jijini Dar es salaam ambao wangependa kuwa sehemu ya tukio la uzinduzi huo

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa ameishukuru klabu ya Simba kwa kushirikiana nao katika kuhakikisha Wanasimba wanapata usafiri bora na nafuu kuelekea Morogoro

"Tutashirikiana na ninyi kwa kwenda na kurudi pamoja Morogoro na hata ukiangalia nauli zetu ni rafiki Tsh. 13,000 tu. Tunawashukuru sana kwa tukio hili, ni tukio la kizalendo, kwa sisi SGR ni jambo kubwa tunahitaji kuonekana," alisema Kadogosa

Nae Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mikumi, Agustino Masesa amewakaribisha Wanasimba Mikumi kwenda kushuhudia Wanyama mbalimbali akiwemo Mnyama Simba

"Simba inakuja Mikumi na Mikumi kuna Simba. Mnakuja kukutana na Simba wa kweli. Tunawakaribisha sana na tunawashukuru sana kwa kutupa heshima ya kuja kuzindulia Simba Week kwenye hifadhi yetu, "alisema Masesa

Gharama ya kuingia mbuga ya Mikumi kufanya utalii wa ndani ni Tsh 5,900/- ambapo Msemaji wa Simba Ahmed Ali amewahamasisha Wanamsimbazi kufanya utalii wa ndani

"Twendeni Hifadhi ya Mikumi tukawaonyeshe Watanznia kuna hifadhi, ni karibu na kiingilio ni 5,900. Kuna wengine wakisikia utalii wanajua ni mamilioni kumbe ni hela kidogo. Lakini pia ni kwenda kutangaza treni mpya ya SGR. Kwanza ni bidhaa mpya ambayo inatakiwa kutangazwa na sisi Simba Sports Club ndio Wenye Nchi kuitangaza"

"Safari yetu itakuwa ni Julai 24, 2024 na treni itaondoka Dar es Salaam saa 12:00 alfajiri, muda wa kufika kituoni ni saa 11:00 alfajiri. Wale wote ambao wanatamani kuungana nasi kuelekea Morogoro kufika kwa wakati. Tutafika Morogoro saa 1:30 asubuhi. Mpaka sasa tumekodi behewa tatu kwa ajili ya Wanasimba na kwa mashabiki wetu hakutakuwa na nauli. Kila shabiki wa Simba ambaye anahitaji kuandika historia kupanda SGR, kufika Mikumi, kushiriki uzinduzi wa Wiki ya Simba afike akiwa na jezi ya Simba"

"Tukifika Morogoro tutakuta Wanasimba wenzetu wamekuja kutupokea. Kwa hili niyashukuru matawi ya Simba Morogoro. Tunataka kwenda kuishangaza Morogoro na ninyi mnatujua sisi sio watu wa kufanya mambo madogo madogo, tunafanya kwa ukubwa wake. Na nichukue nafasi hii kuwambia wakati wa Morogoro anayekwenda kazini awahi mapema kabla ya saa 1:30 asubuhi maana Mnyama akifika atakuwa mtaani kufanya hamasa zake."

"Tutafanya utalii mbugani na baada ya hapo tutacheza mechi tutarudi Morogoro mjini na kuanza sfaari kurudi Dar es Salaam. Hii itakuwa tarehe 24, Julai. Tutakwenda na kurudi lakini kama ukitaka kulala Morogoro unaruhusiwa," alisema Ahmed

ADVERTISE HERE

More Stories

Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
39m ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
13h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
14h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
15h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
15h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
16h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
17h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
20h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
22h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
23h ago
READ MORE β†’