Yanga - Local

Manara amaliza adhabu ya TFF

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Jul 2024
Manara amaliza adhabu ya TFF

Aliyekuwa Msemaji wa Yanga Haji Manara amemaliza kifungo chake cha miaka miwili kilichohusu masuala ya soka

Leo Manara alikwenda kulipa faini ya Tsh Milioni 10 kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na hivyo rasmi sasa yuko huru kuendelea na majukumu yake kama mdau wa soka nchini

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo, Manara alisema yeye bado ni mwajiriwa wa klabu ya Yanga mpaka 2026 hivyo anaisubiri klabu irejee nchini kufahamu kama anaendelea na majukumu yake ya awali au atapangiwa majukumu mapya

Manara amemshukuru Mdhamini/Mfadhili wa Yanga Ghalib Said Mohammed 'GSM' kwa kumlipa mshahara kwa kipindi chote alichokuwa amefungiwa

Aidha Manara amesema mwaka uliopita aliongezewa mkataba ikiwa ni pamoja na kupandishwa mshahara ambapo ataendelea kuwa mwanafamilia wa Yanga mpaka 2026

"Juzi niliwatuma watu wangu kwenda TFF kwa bahati mbaya hawakufanikiwa ila leo asubuhi na mapema walienda tena na risiti za Benki yenye hundi ya Milioni 10 . Tayari nimeshalipa fedha asante kwa wote waliofanikisha hili naomba tuungane ili tuuendeleze mpira wetu"

"Nakumbuka siku ya mwisho nilifungiwa kama Msemaji wa klabu yangu pendwa ya Yanga tayari adhabu yangu imeisha kwasasa nausubiri uongozi urejee nchini. Wote mtafahamu ni majukumu gani nitapangiwa na uongozi baada ya adhabu yangu," alisema Manara

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
2h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
6h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
7h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
8h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
8h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
9h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
9h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
22h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’