Azam - Local

Azam Fc yaahidi burudani baada ya pre-seson

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Jul 2024
Azam Fc yaahidi burudani baada ya pre-seson

Kocha wa Azam FC, Bruno Ferry amewaahidi mashabiki wa timu hiyo soka la kuvutia kutoka nchini Morocco ambako amekuta timu nyingi zinapenda kuuchezea mpira

Akizungumza kutoka nchini humo ambako kikosi cha timu hiyo kimepiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano, Ferry amesema ameona aina fulani ya soka nchini humo ambalo ni la kuvutia na ameanza kuliingiza kwenye kikosi chake kwani kina baadhi ya wachezaji ambao ni mafundi wa mpira miguuni

"Nimeona soka la Morocco ni la kiufundi sana, wanapenda kuchezea mpira, nasi hatuna tatizo na hilo, tunao wachezaji ambao wanaweza kulicheza, kuna vitu ambavyo tunawaongezea wachezaji wetu ili waweze kucheza aina hiyo ya soka la kuburudisha na kuvutia machoni, huku wakisaka ushindi," alisema kocha huyo

Jumamosi iliyopita, Azam FC, ilicheza mchezo wa kwanza wa kujipima nguvu dhidi ya US Yacoub Al Mansour inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu nchini humo na kushinda mabao 3-0

Akizungumzia maandalizi kwa ujumla, alisema bado wachezaji wake hawajafika anapopataka, lakini kazi inaendelea kuwafua ili wawe vizuri

"Bado hatujafika tunapotaka, ila ni hali ya kawaida katika kipindi hiki cha maandalizi, kwa sasa ni muhimu kuendelea na mazoezi ya utimamu wa mwili, ni wakati wa kujiandaa na michezo mbalimbali na kuhakikisha wachezaji wapya wanaingia kwenye mfumo

"Katika soka kuna hasi na chanya, tunajua kila kitu hakiwezi kuwa sawa na vile unavyotaka, vinahitaji muda, nadhani mashindano yatakapoanza tutakuwa tayari," alisema

Mbali na Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam inajiandaa pia na Ligi ya Mabingwa Afrika, ilipangwa kucheza dhidi ya APR ya Rwanda kuanzia Agosti 16 na 18, mwaka huu kabla ya hapo inatakiwa kuikabili Coastal Union, Agosti 8 katika mechi ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa New Amaan Complex, mjini Zanzibar

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’