Simba - Local - Transfer

Simba yapania usajili wa Mpanzu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Jul 2024
Simba yapania usajili wa Mpanzu

Mabosi wa Simba wamelazimika kufungua tena mazungumzo kumsajili kiungo mshambuliaji wa AS Vita Elie Mpanzu ambaye unaweza kusema katika dirisha hili la usajili ndiye mchezaji ambaye tetesi za usajili wake zimezungumzwa kwa muda mrefu zaidi

Baada ya sintofahamu ya Kibu Denis aliyetorokea Ulaya, ni wazi Simba inalazimika kusajili mchezaji wa kuziba nafasi yake

Ili kupata mchezaji wa daraja la juu, Simba inalazimika kuangalia tena nje ya nchi uamuzi ambao pia utawalazimu kuachana na mchezaji mmoja zaidi wa kigeni

Jana tetesi za Simba kurejea tena kwa Mpanzu zikaanza kuvuma ambapo taarifa zilibainisha kuwa Simba iliongeza dau ili kuishawishi AS Vita kumuachia winga huyo ambaye kwa sasa ndiye mchezaji bora wa Vita

Wadadisi wa masuala ya usajili wanasema kuna nafasi kubwa Simba itafanikiwa kumsajili winga huyo ambaye tayari alishafikia makubaliano binafsi juu ya maslahi yake pale atakapojiunga na Simba

Pengine Mpanzu alipaswa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Simba katika dirisha hili lakini ilitokea sintofahamu kuhusu mkataba wake

Mwenyewe alisema amemaliza mkataba na AS Vita lakini klabu hiyo ikakanusha na kuthibitisha kuwa Mpanzu bado ana mkataba wa mwaka mmoja

Changamoto ikawa dau ambalo Vita wanataka ambapo Mnyama atalazimika kutoa zaidi ya Milioni 600 kununua mkataba wake wa mwaka mmoja uliobaki

Wakati huu Simba imerejea ikiwa 'serious' na pengine ile kiu ya Wanamsimbazi kumuona Mpanzu akivaa uzi wa Mnyama inaweza kufanikiwa

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’