Yanga - Local

Kaizer Chiefs, Yanga kuchuana Jumapili

Joel JJ By Joel JJ
27 Jul 2024
Kaizer Chiefs, Yanga kuchuana Jumapili

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema anatarajia mchezo wa Toyota Cup dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa Jumapili, utakuwa maandalizi mazuri kwa kila timu kuelekea msimu mpya wa mashindano

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari ambao ulihusisha makocha wa timu zote, Gamondi alisema mchezo utakuwa na ushindani akiamini Kaizer Chiefs watakuja na ari kubwa kufuatia ujio wa Kocha Nasreddine Nabi

"Mchezo wetu dhidi ya Kaizer Chiefs utakuwa mchezo mzuri na wenye ushindani hasa ukizingatia Chiefs wana Mwalimu mpya na kila mchezaji atapata nafasi ya kumuonyesha Mwalimu uwezo wake na kwetu sisi pia maandalizi yetu yanazidi kuimarika na tunaamini tutakwenda kuwa na mechi nzuri," alisema Gamondi

Aidha Kocha huyo raia wa Argentina amesema maandalizi ambayo Yanga wamepata hapo Afrika Kusini ni faida kubwa kwao lakini pia wameweza kuitangaza Yanga Kimataifa

"Yanga ujio wetu hapa Afrika Kusini umekuwa muhimu sana kwetu kwenye maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2024/25 na kucheza na timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) ni sehemu ya kuendelea kuitangaza Klabu yetu barani Afrika na Duniani kote," alisema

Yanga ilitua Johanesurg jana tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Jumapili katika uwanja wa Toyota

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
56m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
2h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →