Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatano, August 07 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Aug 2024
Tetesi za soka Ulaya, Jumatano, August 07 2024

Arsenal wamesalia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, licha ya kumtaka Paris St-Germain. (Gianluca di Marzio via X)

Brighton wamefanya mawasiliano na mchezaji huru, beki wa zamani wa Bayern Munich na Borussia Dortmund Mats Hummels, 35, ambaye alishinda Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani mwaka 2014, ingawa wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa West Ham. (Sky Sports)

Msako wa Manchester United wa kumtafuta kiungo unaweza kuwafanya watoe ofa ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Norway na Burnley Sander Berge, 26, baada ya klabu hiyo ya Old Trafford kukataa kumsajili mchezaji wa Paris St-Germain raia wa Uruguay Manuel Ugarte, 23. (Athletic - Subscription Required)

Hatahivyo, klabu ya Burnley itahitaji hadi pauni milioni 30 kumnunua kiungo huyo. (Sun)

Barcelona wamefikia makubaliano ya mazungumzo juu ya ada ya £47.3m pamoja na nyongeza ya £6m na RB Leipzig kwa kiungo mshambuliaji wa Uhispania Dani Olmo, 26. (Fabrizio Romano on X)

Tottenham wanavutiwa na mshambuliaji wa Bournemouth Dominic Solanke, lakini uhamisho wa Muingereza huyo unaweza kutegemea mustakabali wa mshambuliaji wa Brazil Richarlison, 27. (Standard)

Spurs wanajiandaa kwa ofa kubwa ya Richarlison kutoka kwa Saudi Pro League. (Football Insider)

Bayern Munich bado hawajafanikiwa katika mazungumzo yao na Bayer Leverkusen kuhusu kumnunua beki wa Ujerumani Jonathan Tah, 28. (Sky Germany)

Brentford wamewasilisha ombi la pauni milioni 7 kumnunua beki wa Burnley kutoka Jamhuri ya Ireland Dara O'Shea, 25. (HITC)

Ajax, Feyenoord na PSV wote wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Coventry City Mholanzi, Milan van Ewijk, mwenye umri wa miaka 23. (ESPN - In Dutch)

West Ham wako tayari kusikiliza ofa kwa mshambuliaji wa Uingereza Danny Ings, 32. (Football Insider)

Kipa wa Aston Villa Muingereza James Wright, 19, yuko kwenye mazungumzo ya kujiunga na Real Union, inayoshiriki ligi ya daraja la tatu Uhispania, kwa mkopo msimu huu. (Athletic - Subscription Required)

Atletico Madrid wako kwenye mazungumzo ya juu na Valencia kuhusu mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Javi Guerra, 21. (Athletic - Subscription Required )

Beki wa Chelsea Muingereza Alfie Gilchrist, 20, anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kujiunga na Sheffield United kwa mkopo wa msimu mzima. (Sky Sports)

BBC

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’