Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jummosi August 10 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Aug 2024
Tetesi za soka Ulaya, Jummosi August 10 2024

Manchester United wanajiandaa kuwasilisha ofa mpya kwa mlinzi wa Everton aliye na umri wa miaka 22 Jarrad Branthwaite - baada ya kubaini kuwa mchezaji wao mpya, mlinzi wa Ufaransa Leny Yoro, 18, hawezi kucheza tena mwaka huu. (Sun)

Beki wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 24, na beki wa Morocco Noussair Mazraoui, 26, wanatarajiwa kujiunga na Manchester United kutoka Bayern Munich huku mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yakiendelea. (Sky Sports Germany)

Bayern Munich wamejiondoa katika mpango wa kumsajili beki wa Ujerumani Jonathan Tah, 28 kutoka Bayer Leverkusen. (Kicker - kwa Kijerumani)

Crystal Palace wamekataa ofa ya pili, inayoaminika kuwa ya takriban £50m, kutoka kwa Newcastle United kwa ajili ya beki wao Marc Guehi, 24, huku mazungumzo yakiendelea kati ya klabu hizo mbili. (Sky Sports)

Bilionea wa Marekani John Textor ametoa ombi la kuwa mmiliki mkubwa wa Everton, jambo ambalo linaweza kumaliza sakata la kuuzwa kwa klabu hiyo. (Guardian)

Mshambuliaji wa Brazil Rodrygo, 23, hana nia ya kuondoka Real Madrid hata kama Manchester City watajaribu kumchukua kama mbadala wa mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, ambaye anatazamiwa kujiunga na Atletico Madrid. (AS - kwa Kihispania)

Crystal Palace wapo kwenye mazungumzo na Galatasaray kuhusu mkataba wa msimu mzima kwa winga wa zamani wa Eagles Wilfried Zaha. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 31 aliondoka katika klabu ya Selhurst Park na kujiunga na klabu hiyo ya Uturuki kwa uhamisho wa bure msimu uliopita. (Guardian)

Leicester City pia wanashughulikia mpango wa kumsajili Zaha kutoka Galatasaray. (Athletic - usajili unahitajika)

Arsenal wako tayari kuidhinisha kuondoka kwa mshambuliaji Muingereza Eddie Nketiah, 25, kwenda Marseille kwa mkopo na watalazimika kununua kwa ada ya pauni milioni 25. (Athletic - usajili unahitajika)

Wolverhampton Wanderers wanamnyatia winga wa Ajax mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ureno Carlos Forbs kuchukua nafasi ya Pedro Neto, 24, ambaye anakaribia kuhamia Chelsea. (Fabrizio Romano)

West Ham United wanakaribia kushinda katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Ufaransa Jean-Clair Todibo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Nice huku kukiwa na ushindani mkali kutoka kwa Juventus. (Telegraph - usajili unahitajika)

Queens Park Rangers wanavutiwa na kiungo mshambuliaji wa Japan mwenye umri wa miaka 22, Koki Saito, ambaye kwa sasa yuko na klabu ya Lommel ya Ubelgiji. (West London Sport)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’