Yanga - Local

Jeuri ya Yanga kwa Mzize iko hapa

Joel JJ By Joel JJ
4 Sep 2024
Jeuri ya Yanga kwa Mzize iko hapa

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mshambuliaji Clement Mzize amechagua kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa nchi kutokana na mipango mizuri waliyonayo

Hivi karibuni Yanga ilipokea ofa kutoka kwa klabu za Wydad Athletic, Kaizer Chiefs na nyingine kutoka barani Ulaya kwa ajili ya mshambuliaji huyo kinda

Hata hivyo Yanga iliweka msimamo na kukataa ofa zote wakisisitiza kuwa mchezaji huyo anahitajika katika kufanikisha 'project' ya Yanga

"Kumbakisha Mzize ni moja kati ya mipango tuliyokuwa nayo katika klabu yetu ya Yanga. Mzize ni mchezaji mzuri sana ambaye tunaamini anaweza kuisaidia Yanga ikafikia malengo yake ambayo ni kutwaa ubingwa wa Afrika"

"Ikitokea hii leo Mzize au mfano hata Aziz Ki amesajiliwa na Al Ahly na timu hiyo ikabeba ubingwa wa Afrika, wao binafsi hawawezi kusema kawapa kombe na haitokuwa ajabu sana kwa sababu wameshatwaa kombe hilo mara 11. Lakini mshawahi kujiuliza kama Mzize anabeba kombe la Afrika na Yanga  kwa mara ya kwanza katika historia ni kitu ambacho kitampa heshima kubwa kama mchezaji"

"Lakini pia sisi tunasema hatumuuzi Mzize kwa sababu tunaweza kumtimizia mahitaji yake. Hatuwezi kuwa na jeuri hiyo kama tusingekuwa na fedha," alitamba Kamwe

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
55m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
2h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →