Yanga imefanikiwa kupata ushindi muhimu ugenini wakiichapa CBE SA bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza raundi ya pili michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Alikuwa ni Prince Dube aliyefunga bao pekee la Yanga dakika ya 45 kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya Pacome Zouzoua
Pengine ulikuwa mchezo ambao Yanga ingeweza kuibuka na ushindi mnono zaidi Dube akikosa nafasi kadhaa katika kipindi cha kwanza huku Maxi Nzengeli, Mzize na Chama nao wakikosa katika kipindi cha pili
Ni ushindi ambao unaiweka Yanga mbele na sasa zimebaki dakika 90 nyingine kumaliza kazi nyumbani