Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili Septemba 15 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Sep 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili Septemba 15 2024

Real Madrid watatuma skauti katika mchezo wa Jumapili wa London kaskazini huku wakifikiria kumnunua beki wa Arsenal mwenye umri wa miaka 23 William Saliba na wa kati wa Tottenham na Argentina Cristian Romero, 26. (Defensa Central)

Winga wa Chelsea mwenye umri wa chini ya miaka 20 wa Chelsea Carney Chukwuemeka ni miongoni mwa walengwa wa AC Milan katika dirisha la uhamisho la Januari. (Calciomercato)

Real Madrid wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili mlinzi wa Bayern Munich Alphonso Davies, 23, kwa uhamisho wa bila malipo, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Canada akiweza kusaini mkataba wa awali wa kandarasi kuanzia Januari. (AS)

Liverpool wanamtafuta mlinzi wa Sevilla Mfaransa Loic Bade, 24, huku wakifikiria kuchukua nafasi ya mlinzi wa kati wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33. (Caught Offside)

Chelsea wanaweza kurejea kumnunua mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen mwenye umri wa miaka 25 mwezi Januari kutokana na kipengeLe cha mapumziko katika mkataba wake wa mkopo huko Galatasaray. (Football Insider)

Barcelona ilikataa ofa ya takribanI pauni milioni 210 kutoka kwa Paris St-Germain kwa winga wa Uhispania Lamine Yamal, 17, mwezi Juni, kulingana na Andy Bara - wakala wa kiungo wa kati wa Barca na hispania Dani Olmo. (Mundo Deportivo)

West Ham wanaendelea kufanyia kazi mpango wa kumsajili beki wa zamani wa Cameroon Joel Matip, 33, kwa uhamisho wa bure. (Football Insider)

Mama na wakala wa Adrien Rabiot anasema kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29, ambaye amekuwa akihusishwa na Newcastle na Manchester United, hatarejea klabu ya zamani ya Juventus. (Mirror)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’