CAF CC: Al Ahly Tripoli vs Simba leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Sep 2024
CAF CC: Al Ahly Tripoli vs Simba leo

Leo Simba inafungua pazia la michuano ya Kimataifa kwa kuikabili Al Ahli Tripoli katika mchezo wa mkondo wa kwanza raundi ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho la CAF

Ni msimu mwingine kwa Simba kuendeleza rekodi yake ya kibabe katika mashindano ya CAF

Baada ya maboresho makubwa na kikosi na ujio wa benchi jipya la ufundi, kocha Fadlu Davids na vijana wake leo wanakwenda kujaribiwa na wajukuu wa hayati Kanali Muammar Gaddafi katika uwanja wa Juni 11

Ni wazi itakuwa mechi ngumu ambayo inazikutanisha timu zenye malengo yanayofanana

Kwa Simba kucheza hatua ya makundi katika mashindano ya CAF ni jambo la kawaida kwani katika miaka sita wametinga makundi mara tano na kucheza robo fainali nne mfululizo

Al Ahli Tripoli nao wamekuwa na mwenendo mzuri katika ushiriki wao wa kombe la Shirikisho kwani mwaka 2022 walifanikiwa kucheza hatua ya nusu fainali na mara kadhaa wamecheza ligi ya mabingwa na kuwahi kufika robo fainali pia

Dimba la Juni 11 litakuwa 'full house' kwani Al Ahli Tripoli wameuza tiketi zote za mchezo huo ambapo takribani mashabiki 60,000 watakuwa uwanjani kushuhudia mchezo huo

Mkufunzi wa Simba Fadlu Davies amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo, hii sio mara ya kwanza kwa Simba kucheza mechi yenye presha kubwa ugenini 

Fadlu amesema watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri lakini jambo la ambalo ana uhakika nalo ni kuwa mechi itamalizikia jijini Dar es salaam

Ni wazi Simba itacheza kwa tahadhari kubwa leo, ili kuhakikisha inashinda au hata kupata sare ili mechi ya nyumbani kusiwe na kazi kubwa ya kufanya

Simba imejijengea heshima kubwa katika soka la Afrika yanapokuja mashindano ya CAF iwe ligi ya mabingwa au kombe la Shirikisho

Hivyo bila shaka, Mnyama leo atadhihirisha kwa nini anashika nafasi ya saba kwa ubora barani Afrika

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
43m ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
2h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
3h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
3h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
5h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
6h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
6h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
18h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’