Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Septemba 17 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Sep 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Septemba 17 2024

Liverpool wanaripotiwa kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Lille Angel Gomes, huku maskauti wa Reds wakihudhuria mchezo wa kwanza wa kuvutia wa mchezaji huyo wa kwanza wa England dhidi ya Finland mwezi huu. (Liverpool Echo)

Crystal Palace na Ipswich wote wanamfuatilia beki wa kushoto wa England na Chelsea Ben Chilwell kabla ya uhamisho wa Januari. (Sun)

Bayern Munich wanatatizika kumshawishi kiungo mkabaji Jamal Musiala, 21, kuongeza mkataba wake na klabu hiyo, jambo ambalo linaweza kuibua nia ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kutoka Manchester City na Manchester United. (Daily Mirror)

Mkufunzi wa Everton Sean Dyche anafikiria kumnunua kipa wa England na Newcastle Nick Pope, 32, kuchukua nafasi ya Jordan Pickford, 30. (Daily Mirror)

Kiungo wa kati wa zamani wa Juventus Adrien Rabiot, ambaye ni mchezaji huru, anakaribia kujiunga na klabu ya Ligue 1 ya Marseille baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 kuhusishwa na klabu za West Ham na Manchester United. (L'Equipe, In French , Subscription Required)

Manchester United wanatarajiwa kumpa winga Amad Diallo, 22, mkataba mpya wa muda mrefu katika miezi ijayo. Mkataba wa sasa wa raia huyo wa Ivory Coast unamalizika msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)

Mlango unaweza kuwa wazi kwa bosi wa zamani Steven Gerrard kurejea Rangers na kuchukua nafasi ya Philippe Clement kama meneja. (Daily Record)

Manchester City inamfuatilia kiungo wa Nottingham Forest Morgan Gibbs-White, 24, lakini Forest wana nia ya kumpa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mkataba mpya. (HITC)

Beki wa kushoto wa Real Madrid na Ufaransa Ferland Mendy, 29, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Uhispania hadi 2027. (Marca – In Spanish)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
55m ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
2h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
3h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
4h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
5h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
6h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
6h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
19h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’