Azam - Yanga - Simba - Local - Transfer

Fei Toto aitega Azam Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Sep 2024
Fei Toto aitega Azam Fc

Klabu ya Azam Fc imefungua mazungumzo ya kumuongeza mkataba kiungo wake Feisal Salum 'Fei Toto', hata hivyo nyota huyo amegomea mazungumzo hayo, imefahamika

Fei Toto bado ana mkataba na Azam Fc unaomalizika mwishoni mwa msimu, matajiri hao kutoka Chamazi wanataka kumpa mkataba wa muda mrefu zaidi kwa kuzingatia ubora alionao sasa

Akihojiwa na wanahabari hivi karibuni katika siku ya Azam Media Day, Fei Toto alifichua yuko tayari kwa changamoto mpya katika klabu nyingine

Fei Toto alisema tayari mezani kuna ofa kutoka klabu mbalimbali lakini kwa sasa anaheshimu mkataba wake na Azam Fc

"Mimi ni mchezaji nacheza popote, iwe Simba, Yanga, Azam na hata nje ya nchi kama nitapata nafasi hiyo"

"Kwa sasa nina mkataba na Azam Fc hivyo naheshimu mkataba huo lakini nafahamu kuna timu zimeonyesha nia ya kunihitaji," alisema Fei Toto

Feitoto pia alikanusha uvumi unaodai kuwa hana maelewano mazuri na Rais wa Yanga Injinia Hersi ambapo kiungo huyo alibainisha kuwa amekuwa akiwasiliana na Hersi mara kwa na ni mtu anayemshauri mambo mengi

"Mimi sina tatizo lolote na Injinia Hersi, ni mtu ninaewasiliana nae mara kwa mara na hunishauri vitu vingi. Hakuna tofauti yoyote kati yangu naye"

Kumekuwa na taarifa kuwa Fei Toto yuko tayari kurejea kwa waajili wake hao wa zamani Yanga, baada ya misimu miwili ya kuitumikia Azam Fc

Klabu ya Simba pia inatajwa kumuwania kiungo huyo tegemeo wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Katika dirisha la usajili lililopita, Simba walifungua mazungumzo na Azam Fc kwa ajili ya kumsajili Fei Toto lakini Azam Fc hawakuwa tayari kufanya biashara

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
4h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
9h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
11h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
14h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
14h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’