Ligi Kuu ya NBC inaendeleo leo kwa michezo miwili kufanyika Kagera na Tabora
Wageni wa ligi hiyo, KenGold ya Mbeya baada ya kupoteza michezo 3 mfululizo, wataikabili Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
KenGold ipo nafasi ya 16 mwisho wa msimamo wa Ligi Kuu na haina pointi wakati Kagera Sugar ambayo nayo inasuasua inashika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 1 baada ya michezo 4
Kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, wenyeji Tabora United itakaribisha Fountain Gate
Tabora United inashika nafasi ya 4 ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 4 wakati Fountain Gate ipo nafasi ya 3 pia ikiwa na pointi 7 pia