Yanga ni klabu pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ikiungana na wababe wengine 15 kutoka pande nyingine za Afrika
Baada ya kucheza fainali ya kombe la Shirikisho 2022/23 na robo fainali ya ligi ya mabingwa 2023/24, Yanga imepaa katika 'ranking' za CAF sasa ikiingia 10 bora
Kuelekea droo ya makundi itakayofanyika Oktoba 07 huko Misri, Yanga itakuwa poti ya pili sambaba na Raja CA, Pyramids na CR Belouizdad. Timu hizi hazitakuna na Yanga katika hatua ya makundi. Wananchi watapangwa dhidi ya timu kutoka poti 1, 3 na 4
Poti 1 ina Al Ahly, Esperance, Mamelodi Sundowns na TP Mazembe
Poti 3 ina Al Hilal, Orlando Pirates, Sagrada Esperanca na AS Far Rabat
Poti 4 ina MC Alger, Djoliba, Stade De Abdijan na Maniema Union




