Yanga - Simba - Azam - Singida - Local

Mambo magumu kwa timu hizi Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Sep 2024
Mambo magumu kwa timu hizi Ligi Kuu

Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikiingia raundi ya tano, jumla ya timu tano bado hazijaonja ladha yoyote ya ushindi

Timu hizi ni Prisons, Pamba Jiji, JKT Tanzania, Coastal Union na KenGold, zimecheza michezo tofauti, zikiwa hazijashinda mechi yoyote ya Ligi Kuu msimu huu

Prisons ambayo iko nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi, imecheza michezo minne bila kushinda, ikitoka sare mechi zote na ina pointi nne

Pamba Jiji, imeshatimiza michezo mitano mpaka sasa ikiwa imepanda daraja msimu huu, lakini haijaonja ladha ya ushindi wa Ligi Kuu, ikitoka sare nne na kupoteza mmoja, ikiwa na pointi nne kwenye nafasi ya 10 ya msimamo

JKT Tanzania imecheza michezo mitatu ambayo yote imetoa sare, ikiwa na pointi tatu na inashika nafasi ya 13

Coastal Union mpaka sasa imeshacheza michezo minne, ikitoka sare moja tu na kupoteza mitatu, ikikamata nafasi ya 15 na KenGold inayoshika mkia, ikiwa imecheza mechi nne, ikipoteza zote na haijavuna pointi mpaka sasa

Singida Black Stars ndiyo timu iliyoshinda michezo yote iliyocheza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka sasa

Timu hiyo imeshinda michezo minne iliyocheza kwenye ligi na kuwa na ushindi wa asilimia 100. Ilianza ligi kwa kuifunga KenGold mabao 3-1, ikaichapa Kagera Sugar bao 1-0, ikapata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC, kabla ya kuifunga Pamba Jiji bao 1-0

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
4h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
4h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
5h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
8h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
12h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
12h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
13h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
14h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
14h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
15h ago
READ MORE β†’