Prisons - Local - Fountain

Prisons yafurahia ushindi wa kwanza Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Oct 2024
Prisons yafurahia ushindi wa kwanza Ligi Kuu

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Mbwana Makata, ameeleza kufurahishwa na ushindi wa kwanza kwa timu yake kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kucheza michezo sita sawa na dakika 540, akisema huo ni mwanzo tu wa mazuri ambayo yanakuja kwenye timu yake

Awali Prisons ilicheza dakika 450 bila kupata ushindi, ikiwa ni michezo mitano, ikitoa sare nne na kupoteza mmoja, kabla ya juzi kupata ushindi wa kwanza wa mabao 3-2, dhidi ya Fountain Gate, ikicheza uwanja wake wa nyumbani, Sokoine jijini Mbeya

Makata, alisema haikuwa rahisi, kwani walikuwa wakitanguliwa kufungwa, lakini mara zote mbili walifanikiwa kusawazisha na hatimaye kupata bao la ushindi

"Niwapongeze wachezaji wangu, wamepambana kwa kila njia, walicheza wakiwa na uchovu mkubwa kwani tulitoka safarini Ruangwa kucheza na Namungo, katika mchezo huu haikuwa rahisi kushinda kwa sababu tulitanguliwa mara mbili"

"Nasema hivi kwa sababu Fountain ni timu ngumu, ina washambuliaji wazuri ambao ukifanya kosa moja wanaweza kukuadhibu," alisema kocha huyo

Hata hivyo alisema amegundua udhaifu sehemu ya ulinzi kiasi cha kuruhusu mabao mawili ambayo kwa upande wake alisema yalikuwa rahisi sana, hivyo anakwenda kulifanyia kazi

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Fountain Gate, Mohamed Muya, aliwapongeza wapinzani wake kwa ushindi na kuwapa pole viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu yake

"Niipongeze timu iliyoshinda, walikuwa kwenye kiwango bora, nawapa pole viongozi, wachezaji wangu na mashabiki waliotoka Manyara kuja Mbeya kushangilia timu yao," alisema kocha huyo

Mabao ya Prisons kwenye mchezo huo yalifungwa na Nurdin Choma kwa mkwaju wa penalti, Ezekia Mwashilindi na Vedastus Mwihambi, huku ya Fountain Gate yakifungwa na Selemani Mwalimu na Kassim Selemani

Matokeo hayo yanaifanya Prisons kufikisha pointi saba katika michezo sita iliyocheza ikiwa kwenye nafasi ya tisa, Fountain Gate inasalia na pointi zake 13, ikiwa kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo

IPP Media

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’