Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema kikosi chake kiko tayari kuendeleza furaha kwa mashabiki kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union hapo kesho
Akizungumza katika Mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Fadlu amesema amefanya maboresho muhimu na kusahihisha makosa yaliyojitokeza katika mechi zilizopita hivyo Wanamsimbazi watarajie soka safi la kushambulia hapo kesho ambalo litaambatana na alama tatu
"Tunaingia katika mechi hii tukihitaji kushinda, ukiangalia michezo minne iliyopita kuna makosa tulifanya ila katika mechi ya kesho tutakuwa bora"
"Lengo letu ni kucheza vizuri, kutawala kwenye maeneo yote na kupata ushindi ili kuendeleza mwanzo mzuri msimu huu," alisema
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, nahodha wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema wamekuwa na wakati mzuri wa kujiandaa na mchezo huo na watakwenda kupambana ili kuhakikisha wanaibua na ushindi
"Maandalizi yamekwenda vizuri, wachezaji tumepokea yale yote mazuri waliyotupa benchi la ufundi na tutaingia katika mechi ya kesho ili kupata alama zote tatu," alisema



