Simba - Local

Fadlu apania kuipeleka Simba robo fainali CAF CC

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Oct 2024
Fadlu apania kuipeleka Simba robo fainali CAF CC

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema haitakuwa kazi rahisi kwa Simba kutinga robo fainali ya kombe la Shirikisho lakini wamejipanga na watahakikisha wanafanikisha malengo hayo

Droo ya makundi ya CAF CC ilifanyika Misri juzi Simba ikipangwa kundi A na timu za CS Sfaxien, CS Constantine na Bravos

"Ni kundi gumu, Bravos ni timu nzuri, CS Sfaxien na CS Constantine zinatoka Afrika Kaskazini ni timu nzuri pia"

"Tuna faida kidogo kwa sababu tulicheza na Al Ahly Tripoli katika hatua iliyopita, hivyo wachezaji wangu wamepata uzoefu juu ya nini tunapaswa kufanya tutakapokwenda Algeria na Tunisia"

"Haitakuwa rahisi kwa sababu wachezaji wetu wengi hawana uzoefu na michuano hii ya CAF, lakini tutakwenda kushindana"

"Lengo letu kuu ni kuhakikisha tunamaliza nafasi ya kwanza katika kundi. Kuna faida ya kumaliza juu katika kundi kwani kwenye robo fainali utacheza dhidi ya timu iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi jingine ingawa haimaanishi itakuwa mechi rahisi," alisema Fadlu

Simba itaanzia nyumbani katika hatua ya makundi ambapo mechi ya kwanza dhidi ya Bravos itapigwa Novemba 27 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’