Klabu ya soka la Coastal Union imetangaza ya kwamba itatumia dimba la Sheikh Amri Abeid lililopo jijini Arusha kwa ajili ya mechi zake za nyumbani za NBC Premier League
Tangu kuanza kwa msimu huu wa 2024/25, Coastal Union ilikuwa ikiutumia uwanja wa KMC Complex, lililopo Dar es Salaam kwa mechi zake za nyumbani
Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga umefungwa kwa ajili ya ukarabati mkubwa