Mapema tu klabu ya Simba imetangaza viingilio kuelekea mchezo wa ligi kuu Kariakoo Derby dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi ijayo, Oktoba 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 11 jioni
Kiingilio cha chini majukwaa ya Mzunguuko ni Tsh 5,000/- huku VIP A ikiwa Tsh 50,000/-
Simba watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaozikutanisha timu zenye upinzani wa jadi katika historia ya soka la Tanzania



