Yanga - Local

Baleke atamba hajaisha makali

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Oct 2024
Baleke atamba hajaisha makali

Mshambuliaji wa Yanga Jean Baleke 'amejipakulia minyama' kwa kusema yeye ni mshambuliaji bora na hataacha urafiki wake na nyavu

Baleke aliyetua Yanga msimu huu kwa mkopo akitokea klabu ya TP Mazembe, ameanza maisha yake na Yanga kwa kusuasua 

Baleke amesema kama mchezaji ataendelea kujifua ili awe bora zaidi na ataisaidia Yanga kila atakapopewa nafasi ya kucheza

"Mimi ni mfungaji bora, nitaendelea kupambana na kuisaidia timu yangu kila nitakapopata nafasi ya kucheza," alisema Baleke

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alimpa Baleke program maalum ya mazoezi kabla ya kuanza kumtumia baada ya kutoridhishwa na 'fitness' yake

Katika moja ya mahojiano yake, Gamondi alibainisha Baleke ni mshambuliaji mzuri lakini alihitaji kumuimarisha katika baadhi ya maeneo

Gamondi alisema ulikuwa ni mpango maalum ulioandaliwa kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye wakati anajiunga na Yanga alikuwa na changamoto ya uzito na alitakiwa apungue kidogo ili aweze  kuendana na kasi ya Yanga

"Tulimpa programu maalum ili kumuongezea wepesi wa kufanya uamuzi akiwa karibu ya lango na kufunga zaidi ya alivyozoeleka"

"Pia mjue kabisa Baleke ni mahiri zaidi kwa kufunga mabao ya kichwa kuliko miguu, tunataka awe na uwiano mzuri wa kufunga mabao ya aina zote” 

"Mshambuliaji mzuri ni yule ambaye anaweza kufunga kwa mipira ya aina zote juu na chini, kwani kazi yake kubwa ni kuipa timu matokeo ndio maana tunamnoa zaidi, lakini sio kama nina tatizo naye, wachezaji wote kwangu ni wachapakazi, kikubwa natafuta matokeo zaidi kuliko jina la mtu," alisema Gamondi

Baleke tayari amekamilisha program maalum aliyokuwa amepatiwa na Gamondi alimtumia kwa takribani dakika 60 katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0

Baleke ndiye aliyesababisha bao la pili lililofungwa Stephane Aziz Ki kupitia mkwaju wa penati baada ya kuvutwa ndani ya eneo la hatari

Angeweza kuondoka na bao lake siku hiyo kama sio uimara wa mlinda lango wa Pamba Jiji Yona Amos aliyeokoa moja ya michomo hatari iliyopigwa na Baleke mwanzoni mwa kipindi cha pili

Mwenyewe ameahidi kama atapata nafasi ya kucheza katika mchezo dhidi ya Simba Oktoba 19, basi atapeleka kilio kwa waajiri wake hao wa zamani

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
38m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
51m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’