Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Oktoba 15 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Oct 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Oktoba 15 2024

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola, 53, amevutiwa na hatua za shirikisho la Soka nchini England kumtaka kuwa meneja wake huku kocha huyo wa Manchester City akitarajiwa kuamua kuhusu mustakabali wake wiki zijazo. (Times)

Guardiola pia anafikiria kusaini mkataba wa mwaka mmoja kusalia City. (Telegraph), Kocha wa muda wa England Lee Carsley ameambiwa hatapata kazi ya kudumu ya England. (Sun)

Newcastle United wanapanga kukubali ofa ya kiungo wa Paraguay Miguel Almiron, 30, mwezi Januari katika jaribio la kutafuta fedha za kuwekeza tena kwenye kikosi chao. (Football Insider)

Liverpool wanavutiwa na mlinzi Loic Bade kama mbadala wa nahodha wao wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33. Hata hivyo, Sevilla haitasikiliza ofa za chini ya euro 20m kwa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Manchester United imekuwa ikimfuatilia kwa karibu winga wa Crystal Palace Eberechi Eze, 26, huku idara ya skauti ya klabu hiyo ikimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza katika msimu mzima uliopita. (Football Transfers)

United inaweza kumsajili tena beki wa kushoto wa Uhispania chini ya miaka 21 Alvaro Carreras, 21, ambaye aliondoka Old Trafford na kwenda Benfica msimu wa joto. (Mirror)

Barcelona wameonyesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Ghana Thomas Partey, 31, huku wakitafuta soko huria la usajili wa wachezaji wapya. (Goal)

Mshambuliaji wa Uingereza Chloe Kelly, 26, anaweza kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu huu baada ya kuona uhusiano wake na meneja Gareth Taylor ukidorora. (Mail)

Hatua zinachukuliwa na kampuni ya usimamizi wa michezo ya A22 kuzindua Super League mnamo Septemba 2025. (AS – In Spanish)

Kiungo wa kati wa zamani wa Ufaransa Paul Pogba, 31, anastahili kurejea Machi 2025 baada ya kutumikia marufuku iliyopunguzwa ya dawa za kusisimua misuli lakini kuna uwezekano wa kuchezea Juventus tena. (Fabrizio Romano)

Pogba amekataa mpango wa klabu ya Broke Boys FC ya Urusi. (French Soccer via Mail)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’