Transfer - International

Tetesi za usajili Jumatano, Oktoba 16 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Oct 2024
Tetesi za usajili Jumatano, Oktoba 16 2024

Manchester City wanamfikiria kocha mkuu wa Sporting Ruben Amorim, 39, kuwa meneja wao mpya ikiwa Pep Guardiola, 53, ataondoka mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. {Guardian) Beki wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 23, analengwa na Manchester United msimu ujao. (Sky Germany)

Barcelona wanaweza kuwalenga kiungo wa Ubelgiji Romeo Lavia na kiungo mshambuliaji wa Uingereza Carney Chukwuemeka, wote 20, kutoka Chelsea mwezi Januari. (Sport – In Spanish)

Mshambulizi wa Uswidi Alexander Isak, 25, ameviweka vilabu vikiwemo Arsenal katika hali ya tahadhari huku akiendelea kusuasua kusaini kandarasi mpya huko Newcastle. (talkSPORT)

Kiungo wa kati wa Senegal Cheikhou Kouyate, 34, alifanyiwa vipimo vya afya huko Leeds Jumanne kama mchezaji huru baada ya kuondoka Nottingham Forest. (Football Insider) 

Paris Saint-Germain bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 26, kutoka Manchester United baada ya mbinu yao ya . (TeamTalks) Chelsea haiko tayari kukaribisha ofa kwa mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 26, huku akihusishwa na Paris St-Germain. (Football Insider)

Tottenham na Crystal Palace zote zinamtaka winga wa Lille mwenye umri wa miaka 21 na Iceland Hakon Arnar Haraldsson. (Football Transfers)

Kipengele cha kutolewa kwa mlinda mlango wa Espanyol Mhispania Joan Garcia, 23, ambaye alikuwa anatakiwa na Arsenal majira ya joto, kimepunguzwa hadi euro 25m (£20.83m). (Mundo Deportivo – In Spanish)

Manchester City huenda ikadai ada ya uhamisho wa rekodi ya dunia kwa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 24, kujiunga na Real Madrid au Barcelona. (Teamtalks)

Wakati huo huo, City wameungana na Chelsea, Arsenal na Tottenham kumfuatilia kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Georgiy Sudakov, 22. (I Sport)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
30m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’