Singida - Local

Singida BS inautaka ubingwa msimu huu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Oct 2024
Singida BS inautaka ubingwa msimu huu

Singida Black Stars imesema imeshaonja 'utamu' wa kukaa kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Bara hivyo haitakuwa rahisi kushushwa kwa sababu wanataka kuendelea kung'ang'ania kwenye nafasi hiyo kwa kupata ushindi watakapocheza dhidi ya Namungo Jumapili kwenye Uwanja wa Liti mkoani, Singida

Singida Black Stars iko kileleni ikiwa na pointi 16 lakini imecheza michezo mingi zaidi ikifuatiwa na Simba yenye pointi 13 sawa na Fountain Gate FC huku mabingwa watetezi, Yanga yenye pointi 12 wakiwa nafasi ya nne

Ofisa Habari wa Singida Black Stars, Hussein Massanza, amesema jana, wamepata bahati kubwa ya kukaa kwa muda mrefu kileleni huku ligi ikisimama kutokana na Kalenda ya Kimataifa, wanataka kubakia kwenye nafasi hiyo na wataonyesha vitendo kwa kuwafunga Namungo

"Tunashauku ya kuhakikisha tunaendelea kuongoza ligi kwa muda mrefu na hata hadi mwisho wa msimu, tumekuwa huko tangu mapumziko ya kalenda ya FIFA, hiyo ni hamasa tosha kwa wachezaji, tumeshawaambia kukaa namba moja si kazi, kuhakikisha tunaendelea kukaa pale ndiyo kazi kubwa," alisema Massanza

Alitamba wamejipanga vyema kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo ili kutengeneza wigo kwa timu nyingine ambazo zinawakimbiza

"Tunajiandaa kwenda kutafuta pointi tatu dhidi ya wageni wetu Namungo, tutacheza kwenye uwanja wa nyumbani hivi sasa maandalizi yanaendelea," Massanza alisema

Singida Black Stars ambayo imeshinda mitano na sare moja, ikifunga magoli tisa na kuruhusu nyavu zake kuguswa mara tatu

Timu hiyo pia inaongoza kwa kuzoa pointi nyingi zaidi kuliko timu yoyote ya Ligi Kuu ikicheza viwanja vya ugenini, ikijizolea pointi 12, ambapo imecheza michezo minne nje ya nyumbani kwake, Liti Singida, ikishinda yote, huku michezo miwili ya nyumbani ikishinda mmoja na sare moja

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
43m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’