Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema hana wasiwasi wowote kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na wanahabari mapema leo, Fadlu amesema kikosi chake kiko kamili wachezaji wote waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa wakiwa wamerejea kuelekea mazoezi ya mwisho leo
"Tunakwenda kucheza mechi ya ushindani dhidi ya Yanga. Natambua Yanga ni timu nzuri ndio maana wametwaa ubingwa kwa misimu mitatu mfululizo"
"Tumejiandaa vyema kucheza mechi hii, tumefanya tathmini ya kina kuhusu wapinzani wetu, tunafahamu vile watakuja katika mchezo huo na sisi tumejiandaa kukabiliana nao"
"Hatuwahofii, Simba ni timu kubwa hivyo tutacheza kama timu kubwa. Aina yetu ya soka ni kushambulia na kuutawala mchezo"
"Huu ni mchezo ambao mshindi sio tu yule atakayekuwa na mbinu bora bali pia atakayekuwa na wachezaji ambao wako tayari kujitoa kwa nguvu za ziada"
"Tunajua mechi zetu dhidi ya Yanga katika Ligi Kuu kuna pointi 6 na kwa malengo yetu sisi Simba tutahakikisha tumezipata zote, haitokuwa rahisi lakini tumejipanga kushinda hiyo mechi, tulipoteza Ngao ya Jamii lakini hii mechi tutafanya vizuri," alisema Fadlu



