Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili Oktoba 20 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Oct 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili Oktoba 20 2024

Manchester City wako tayari kumuuza mlinzi Kyle Walker, Bournemouth wanataka "pesa nyingi" kwa ajili ya beki Milos Kerkez na Liverpool wanatafuta mbadala wa Virgil van Dijk

Manchester City wako tayari kumuuza nahodha Kyle Walker, 34, kwa takriban £15m msimu ujao wa joto. Beki huyo wa Uingereza analengwa na klabu ya Al-Ahli ya Saudi Arabia. (Daily Star)

Manchester City na Liverpool zinaonyesha nia ya kumnunua fowadi wa Brighton Muargentina Facundo Buonanotte, 19, ambaye yuko kwa mkopo Leicester City. (Fichajes - in Spanish) Bournemouth itataka "pesa nyingi" ikiwa ni watilie maanani kumuuza beki wa Hungary Milos Kerkez, 20, ambaye anavutia Liverpool, Arsenal na Manchester United. (Football Insider)

Liverpool wamemlenga beki wa Borussia Dortmund na Ujerumani Nico Schlotterbeck, 24, kama mbadala wa Virgil van Dijk iwapo Mholanzi huyo ataondoka katika klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Caught Offside)

Arsenal wametiwa moyo iwapo wanataka kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth Antoine Semenyo, 24, baada ya kusema yeye ni shabiki wa Gunners na anataka kucheza soka ya Ligi ya Mabingwa. (Football 365)

Manchester United huenda ikamsajili tena beki wa kushoto Alvaro Fernandez, 21, ambaye alijiunga na Benfica kwa mkataba wa kudumu msimu wa joto na anafuatiliwa na Liverpool na Real Madrid. (Teamtalk)

Barcelona wameanzisha mazungumzo ya mkataba kuhusu makubaliano mipya kwa mlinzi Ronald Araujo, 25 - anayelengwa na Manchester United na Chelsea - na kiungo Frenkie de Jong, 27, ambaye pia anasakwa na Red Devils. (90 min)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 31, anaonekana kutokuwa na uwezekano wa kuichezea tena Juventus mara tu marufuku yake ya kutumia dawa za kusisimua misuli itakapokamilika mwezi Machi baada ya mkurugenzi wa klabu kusema kuwa kikosi kimekamilika bila yeye. (DAZN, via ESPN)

Meneja mpya wa England Thomas Tuchel atapokea marupurupu ya pauni milioni 3 ikiwa anaweza kuiongoza Uingereza kushinda Kombe la Dunia la 2026. (The Sun)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
30m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’