Yanga yaichapa JKT Tanzania 2-0

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd October 2024


Yanga yaichapa JKT Tanzania 2-0

Yanga imeendelea kugawa dozi katika ligi kuu ya NBC leo ikiichapa JKT Tanzania mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex

Mabao ya kipundi cha kwanza yaliyofungwa na Pacome Zouzoua na Clatous Chama yalitosha kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu ambazo zimewarudisha katika  nafasi ya pili

Ni ushindi wa 6 mfululizo kwa Yanga kwenye ligi huku Wananchi wakiwa wamefunga mabao 11 pasipo kuruhu nyavu zao kutikiswa

Yanga ndio timu pekee ambayo haijaruhusu bao, mlinda lango Djigui Diarra akiwa na cleensheet 6


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.