Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano, Oktoba 23 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Oct 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano, Oktoba 23 2024

Kocha wa zamani wa Barcelona Xavi amefanya mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kuchukua nafasi ya Erik ten Hag. (Mail)

Sevilla wana nia ya kumsajili beki wa Tottenham mwenye umri wa miaka 18, Archie Gray kwa mkopo. (Mucho Deporte - kwa Kihispania)

Chelsea imemwambia mlinzi wa umri wa miaka 18 wa England Josh Acheampong kwamba hataichezea klabu hiyo kwa kiwango chochote tena hadi asaini mkataba mpya. (Athletic - Usajili unahitajika)

Tottenham wameweka bei ya pauni milioni 80 kwa beki wa Uhispania Pedro Porro, 25, ambaye anawindwa na Manchester City. (Football Insider)

Brighton na Arsenal wanavutiwa na kipa wa Aston Villa wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 21 raia wa Poland Oliwier Zych. (Telegraph - usajili unahitajika)

Kocha wa Arsenal wa timu ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 18 Jack Wilshere, 32, atajiunga na Norwich kama mkufunzi wa kikosi cha kwanza wiki hii baada ya klabu hizo mbili kukubaliana ada ya fidia kwa kiungo huyo wa zamani wa Gunners. (Standard)

Graham Potter, David Moyes na Gareth Southgate wanatarajiwa kurithi mikoba ya Oliver Glasner iwapo atatimuliwa na Crystal Palace. (Guardian)

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Edin Terzic atawania kazi katika klabu ya West Ham iwapo The Hammers watamfukuza Julen Lopetegui. (Florian Plettenberg)

Dortmund wanataka kumsajili beki mwezi Januari huku mchezaji wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27 Ben Chilwell na mchezaji wa kimataifa wa Hungary na Bournemouth Milos Kerkez, 20, wakijumuishwa kwenye orodha yao fupi. (Team Talk)

Wachezaji wakuu barani Ulaya henda wakakataa kutangaza Kombe la Dunia la Vilabu lililopanuliwa hivi karibuni kama sehemu ya mzozo kati ya vyama vya wachezaji na Fifa kuhusu kalenda ya soka iliyosongamana. (Times- usajili unahitajika)

Mpango wa Freidkin Group wa kuinunua klabu ya Everton unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba, lakini wamiliki hao wapya hawataidhinisha matumizi makubwa ya Januari kwa sababu ya vikwazo vya PSR. (The i - Usajili unahitajika)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’