Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Oktoba 24 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Oct 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Oktoba 24 2024

Manchester City wanatazamia kumnunua mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, kama mbadala wa muda mrefu wa Erling Haaland. (Sky Sport Switzerland, via Mirror)

Kocha wa zamani wa Barcelona Xavi anataka kumleta Trafford winga wa Brazil Raphinha mwenye umri wa miaka 27 ikiwa atachukua nafasi ya Erik ten Hag kama mkufunzi wa Manchester United. (Fichajes - kwa Kihispania)

Winga wa Manchester United Mbrazil Antony, 27, anaweza kupewa fursa ya kutoka Old Trafford na klabu yake ya zamani Ajax, lakini wababe hao wa Uholanzi wanasemekana hawajaridhishwa na mpango huo. (De Telegraaf, kupitia Mirror)

Aston Villa wako tayari kumpa mlinda lango wa Poland Oliwier Zych mwenye umri wa miaka 20 kandarasi mpya huku Arsenal na Brighton wakiripotiwa kumtaka. (Football Insider)

Barcelona wanamfuatilia mshambuliaji wa River Plate raia wa Argentina, Felipe Esquivel, 16. (Sport - kwa Kihispania)

Real Madrid wanapanga kumpa beki wa Liverpool na England Trent Alexander-Arnold, 26, kandarasi ya kati ya euro milioni 14-15 kwa mwaka hadi msimu wa 2029-30. (Caught Offside)

Pep Guardiola ameiomba Manchester City kumfuatilia beki wa RB Leipzig Castello Lukeba, 21, huku mkufunzi huyo wa Manchester City akitamani kumnunua Mfaransa huyo msimu ujao. (Fichajes - kwa Kihispania)

Barcelona na Arsenal wanavutiwa sana na mshambuliaji wa Colombia na Aston Villa Jhon Duran, 20, na The Gunners wanaweza kuwa katika nafasi nzuri zaidi kumsajili. (Fichajes - kwa Kihispania)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
7h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
9h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
10h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
10h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
11h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
14h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
16h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
17h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
17h ago
READ MORE β†’