Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Oktoba 25 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Oct 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Oktoba 25 2024

Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland, 24, ana nia ya kujiunga na Real Madrid atakapoondoka katika klabu yake ya sasa, huku kandarasi ya kiungo wa Norway ikikamilika 2027. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Arsenal na Liverpool bado wana nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid Arda Guler, 19, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki akiendelea kutatizika kupata nafasi ya kucheza msimu huu. (CaughtOffside)

Arsenal huenda wakajiunga na mbio za kumsajili mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Victor Gyokeres, 26, huku kocha Mikel Arteta akilenga kuimarisha safu yake ya ushambuliaji. (GiveMeSport)

Mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, ana nia ya kusaini mkataba mpya wa muda mrefu zaidi ya 2028 katika klabu ya Newcastle, licha ya Arsenal na Chelsea kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (i Sport)

Mshambuliaji wa Manchester United Joshua Zirkzee, 23, anaweza kurejea kwa mkopo Serie A baada ya kufunga bao moja pekee katika mechi 11 akiwa na Man United. (Tuttosport viaTeamTalk)

Besiktas wanapania kumnunua mshambuliaji wa Everton Dominic Calvert-Lewin, 27, kwa mkopo, huku Newcastle, Arsenal na Manchester United pia wakimtaka Muingereza huyo. (Fotomac katika Kituruki)

Makocha wa Uingereza Graham Potter na Gareth Southgate ni miongoni mwa wanaowania kuchukua nafasi ya mkufunzi wa Crystal Palace Oliver Glasner ikiwa kiwango cha Eagles hakitaimarika chini ya Muuastria huyo. (TeamTalk)

Arsenal wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Juventus Dusan Vlahovic, 24, ambaye hapo walijaribu kumsajili mwaka 2022. (Caught Offside)

Wakurugenzi wa Barcelona wamekutana na wakala wa kiungo wa kati wa Uhispania Pedri, 21, kujadili hali ya kandarasi yake, ambayo bado haijatatuliwa. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Middlesbrough wameondoa uwezekano wa kiungo wa kati Muingereza Hayden Hackney, 22, kujiunga na Newcastle United au Tottenham Hotspur mwezi Januari. (NipeSport)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
29m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’