Mchezo wa tatu ligi kuu ya NBC leo Ijumaa Oktoba 25 umehitimishwa dimba la Azam complex kwa wenyeji Azam Fc kuibuka na ushindi wa mabao 4-1
Bao la mkwaju wa penati kutoka kwa Feisal Salum 'Fei Toto' na mabao mengine yaliyofungwa na Jhonuer Blanco, Gibril Silllah na Cheikh Cidibe yalitosha kuihakikishia Azam Fc alamu tatu muhimu ambazo zimewasogeza hadi nafasi ya nne katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 18
Jahazi la KenGiold linazidi kuzama, timu hiyo imeendelea kusalia mkiani mwa msimamo wa ligi ikikusanya alama nne tu baada ya mechi 9
Ni wazi wageni hao wa ligi kuu ya NBC msimu huu wanaweza kurejea Championship kama hawataanza kukusanya alama zaidi katika mechi zao
