Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ikiingia mzunguuko wa 10 mechi mbili zikitarajiwa kupigwa katika viwanja tofauti
Baada ya kuchezea kichapo katika derby ya pacha, Fountain Gate watakuwa nyumbani Manyara kuumana na Mashujaa Fc mchezo ukitarajiwa kupigwa saa 10 jioni
Namungo Fc ambao pia walipoteza mchezo uliopita dhidi ya Simba, wamerejea nyumbani uwanja wa Majaliwa kuikaribisha Pamba Jiji mchezo utakaopigwa saa 1 usiku






