Kocha Mkuu wa Singida Black Stars Patrick Aussems amesema ubora wa uwanja wa New Amaan Complex utawapa faida kimbiinu katika mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumatano usiku
Akizungumza katika Mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Aussems alisema kikosi chake kina wachezaji wengi bora hivyo kesho itakuwa nafasi nzuri kwao kuonyesha walichonacho
"Tunatumia uwanja wa LITI kule Singida ambao hauna ubora kama uwanja huu wa Amaan. Naamini kucheza hapa ni faida kwetu kwani tuna wachezaji wengi wazuri ambao wako tayari kucheza dhidi ya Yanga"
"Itakuwa mechi ya wazi ambayo inazikutanisha timu zilizofanya vizuri mpaka sasa. Sote hatujapoteza mchezo wenzetu hawajaruhusu bao, nikuhakikishie itakuwa mechi yenye ushindani mkubwa," alisema Aussems
Nae Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo licha ya changamoto ya ratiba ya kucheza mechi mfululizo
"Kwanza nina furaha kurejea tena hapa Zanzibar, kila Yanga inapokwenda huwa inategemea Ushindi, tupo hapa kwaajili ya Kushinda ingawa tunatambua Singida wana Kikosi kizuri na wamepata muda mrefu wa Kujiandaa," alisema Gamondi