Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, Manchester United na Sporting wamekubaliana kila kitu kuhusu uhamisho wa kocha Ruben Amorim
Ruud van Nistelrooy ataendelea kuiongoza Manchester Unite kama kocha wa muda hadi Novemba 11 kisha wakati wa enzi mpya ya Amorim utaanza
Meneja huyo raia wa Ureno ataongoza mechi yake ya kwanza Novemba 24 dhidi ya Ipswich Town
Mkataba wake na Man Utd ni hadi Juni 2027, Sporting watapokea thamani kamili ya kifungu cha kununua mkataba chenye thamani ya pauni 10m
Zaidi ya hayo, Sporting itapata pauni 1m ya ziada kwa wafanyakazi na notisi ya siku 30 ya kuondoka kwa Amorim iliyokubaliwa katika saa 24 zilizopita