Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, Fountain Gate, Singida BS

Stars yaipania Sudan kufuzu CHAN

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Nov 2024
Stars yaipania Sudan kufuzu CHAN

Kikosi cha Taifa Stars kinaendelea kujifua kwa ajili ya mechi ya marudiano ya kuwania fainali za michuano ya Mabingwa wa Afrika (CHAN) dhidi ya Sudan, huku yakitengenezwa mazingira ya kuwamaliza Wasudani walioshinda mechi ya kwanza kwa bao 1-0

Stars ilifungwa bao katika mechi iliyopigwa wikiendi iliyppita huko Mauritania ikiwa ni mchezo wa raundi ya kwanza na Jumapili hii inahitaji kushinda ili isonge mbele licha ya kuwa na uhakika wa kuwa wenyeji wa fainali hizo za mwakani zitakazofanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda

Katika kuhakikisha Stars inawazima Wasudani, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza mchezo huo ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa hautakuwa na kiingilio

Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, amefafanua umuhimu wa Taifa Stars kupigania nafasi yake kimchezo

"Pamoja na kwamba tayari tunayo nafasi kama wenyeji, lakini kwetu ni muhimu kufuzu kwa kushinda ili kujiweka katika kundi la kwanza na kuweza kukwepa timu ngumu," alisema Ndimbo, aliyefafanua kikosi kipo tayari kwa mchezo huo wa marudiano

Katika mchezo wa awali dhidi ya Sudan uliofanyika Mauritania, Taifa Stars ilipoteza kwa bao 1-0. Hii ina maana kuwa Stars inahitaji ushindi wa angalau mabao 2-0 ili kufuzu hatua inayofuata ikiwa tayari na tiketi ya kushiriki CHAN 2025 kama mwenyeji

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’