Kocha wa Taifa Stars Bakari Shime amewataka mashabiki kufika kwa wingi Uwanja wa Mkapa kesho Jumapili, Novemba 03 kwa ajili ya kuipa nguvu timu yao katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za CHAN dhidi ya Sudan
Shime amesema ni ngumu kueleza namna walivyocheza wakiwa ugenini mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Mauritania, lakini kuna nafasi kwa Watanzania kwenda Uwanjani kwa kuona uwezo wa Taifa Stars ambayo amesisitiza imejiandaa kupata ushindi nyumbani
Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Sudan, Stars ilipoteza kwa kufungwa 1-0
Hakuna kiingilio katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 1 usiku