Ni Mbeya Derby leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 3rd November 2024


Ni Mbeya Derby leo

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mchezo mmoja utapigwa mkoani Mbeya

Ni Mbeya Derby, Tanzania Prisons ikiwa mwenyeji wa KenGold katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine saa 10 jioni

Prisons na KenGold zote zimekuwa na mwanzo mbaya msimu huu ambapo zote ziko katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi

Prisons wanashika nafasi ya 13 wakiwa na alama 7 wakati KenGold wako nafasi ya 16 (mkiani) wakiwa na alama 5

Kila timu inaangalia mechi hii kama nafasi ya kuibuka na ushindi na kuondoka katika eneo la hatari


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.