International,Transfer News,

Tetes za usajili Ulaya, Jumanne Novemba 05 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Nov 2024
Tetes za usajili Ulaya, Jumanne Novemba 05 2024

Inter Milan na Barcelona wanapanga kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Argentina Enzo Fernandez, 23, ambaye mustakabali wake Stamford Bridge haujabainika. (Sun)

Arsenal wamemtambua mshambuliaji wa Newcastle Alexander Isak, 25, kama lengo lao kuu la uhamisho, ingawa Magpies wanadai ada ya takriban pauni milioni 100 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswidi. (Team Talk)

Manchester United wanamtaka winga wa Sporting Geovany Quenda, 17, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno chini ya miaka 21 pia akilengwa na Manchester City, Liverpool na Juventus. (Team Talk)

Kocha wa Manchester United aliyetimuliwa Erik ten Hag hakutaka kumnunua mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee kutoka Bologna msimu wa joto na alikasirika wakati ulipowasili kwa ajili ya kufanya mazoezi. (Sun)

Tottenham wanavutiwa na kiungo wa kati wa Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, lakini hawana uwezo wa kumnunua kutoka AC Milan mwezi Januari. (Football Insider)

Chelsea hawana nia ya kumuuza mlinzi Benoit Badiashile, 23, huku beki huyo wa Ufaransa akizingatiwa kuwa sehemu ya mipango yao ya muda mrefu. (Fabrizio Romano)

Nottingham Forest ingependa kumchukua winga wa Bayern Munich Mathys Tel, 19, kwa mkopo lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa wa chini ya miaka 21 hana mpango wa kuondoka Bavaria msimu huu wa baridi. (Sky Germany)

Kocha wa zamani wa Chelsea na Everton, Frank Lampard, ameibuka kama mgombea anayepigiwa upatu kuchukua mikoba ya mkufunzi Ivan Juric anayekabiliwa na shinikizo ikiwa Roma itaamua kumfuta raia huyo wa Croatia. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Tottenham watazingatia chaguo la mwaka mmoja kwenye kandarasi ya mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min, 32. (Telegraph - usajili unahitajika)

Manchester United itampa kocha mpya Ruben Amorim usemi kabla ya kufanya maamuzi ya kandarasi kuhusu wachezaji wanaokaribia mwisho wa mikataba yao. (ESPN)

Aston Villa wanakaribia kuafikiana kandarasi mpya na mshambulizi Muingereza Morgan Rogers, 22. (Football Insider)

Edu anatazamiwa kuchukua jukumu la mtandao wa vilabu vinavyodhibitiwa na mmiliki wa Nottingham Forest Evangelos Marinakis baada ya kujiuzulu kama mkurugenzi wa michezo wa Arsenal. (Times- usajili unahitajika)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’