Local,Normal News,Azam, Yanga

Azam Fc yataja sababu ya kusherehekea kuifunga Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Nov 2024
Azam Fc yataja sababu ya kusherehekea kuifunga Yanga

Klabu ya Azam FC, imesema inaendelea kusherehekea ushindi wao wa bao 1-0 ilioupata Jumamosi iliyopita dhidi ya Yanga na itafanya hivyo hadi Novemba 23, mwaka huu, itakapocheza mechi yake nyingine ya Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar

Ofisa Habari wa timu hiyo, Hasheem Ibwe, jana alisema kwa bahati nzuri baada ya kuwafunga Yanga hawana mchezo mwingine wowote hadi Novemba 23 itakapocheza dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, hivyo wataendelea kuutumia muda huo kuendelea kusherehekea ushindi huo

Aliwataka wanaowabeza kuendelea kushangilia ushindi huo wawaache kwani wanafanya hivyo si kwa sababu wameifunga Yanga, bali pia wamechukua pointi tatu kwa timu wanayogombea nayo ubingwa, vile vile kuwalipia kisasi wote ambao walifungwa na timu hiyo

"Sherehe zetu bado zinaendelea tangu Jumamosi tumeendelea kufurahia ushindi dhidi ya Yanga, hakuna wa kutupangia ziendelee hadi lini, vibonzo na utani kwenye mitandao ya kijamii vitaendelea kuwapo, wasituchoke, hayo maumivu wanayopata ndiyo ambayo huwa wanayapata wenzao wanapowafunga"

"Tunafanya hivi kwa sababu si tu kwamba tumeifunga Yanga, lakini tumewafunga Mabingwa Watetezi kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, tumeifunga timu ambayo inausaka ubingwa, ukiwa unatafuta ufalme wa soka lazima umfunge yule mnaousaka naye, unakuwa umeshampunguza nguvu na wewe umechukua pointi tatu kutoka kwake"

"Pili Yanga ndiyo mtemi wa wengine, amezifunga timu nyingi tena kubwa, halafu ni timu ambayo ilikuwa haijapoteza mchezo wowote na haijaruhusu bao, yote hayo sisi tumetibua rekodi, kwa nini tusisherehekee wiki nzima?" Alitamba Ibwe

Alisema sherehe hizo zitaendelea hadi Novemba 23, huku wakiwa wamewapa mapumziko wachezaji wao, lakini watarejea tena kwa ajili ya kuanza mazoezi kujiandaa na michezo miwili ya Novemba

"Baada mechi dhidi ya Yanga, tuna michezo miwili mwezi huu, Novemba 23 dhidi ya Kagera Sugar na Novemba 27 dhidi ya Singida Black Stars, ni michezo migumu, lakini wachezaji wetu kwa sasa wana ari ya ushindi," alisema

Azam iliyokuwa mgeni kwenye Uwanja wao wa Azam Complex kikanuni, ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, lililowekwa wavuni na Gibiril Sillah na kuifanya kufikisha pointi 21 kwa michezo 10 iliyocheza ikiwa kwenye nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’