Ethiopia vs Tanzania kupigwa Kinshasa

Joel JJ By Joel JJ β€’ 7th November 2024


Ethiopia vs Tanzania kupigwa Kinshasa

Kikosi cha Tanzania 'Taifa Stars' kinahitimisha mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon 2025 dhidi ya Ethiopia na DR Congo

Tanzania itaanzia ugenini DR Congo kuikabili Ethiopia Novemba 16 katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Marty's Kinshasa

Ethiopia wamechagua kutumia uwanja huo katika mechi zao za mwisho dhidi ya Tanzania na DR Congo

Novemba 19 Tanzania itahitimisha kampeni yake nyumbani dimba la Mkapa kwa mchezo dhidi ya Guinea

Tanzania inapaswa kushinda mechi zote mbili ili kufuzu michuano hiyo itakayofanyika Morocco

DR Congo tayari wamefuzu kutoka kundi H wakiwa na alama 12 baada ya kushinda mechi zote nne

Guinea wako nafasi ya pili wakiwa na alama 6 wakati Tanzania iko nafasi ya tatu ikiwa na alama nne

Ethiopia wanaburuza mkia wakiwa na alama moja


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.