Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Novemba 08 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Nov 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Novemba 08 2024

Liverpool wanaandaa dau la pauni milioni 50 kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 24. (Fichajes - kwa Kihispania)

Juventus wanamtaka mshambuliaji wa Lille Jonathan David, lakini klabu hiyo ya Serie A inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester United, Liverpool na Arsenal kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Canada mwenye umri wa miaka 24. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Manchester United wamefufua tena mpango wa kumnunua beki wa Everton mwenye thamani ya pauni milioni 70, Jarrad Branthwaite, huku klabu hiyo ya Merseyside ikishindwa kumudu kandarasi mpya kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 22. (Mail - usajili unahitajika)

Brighton na Bayer Leverkusen ni miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa na beki wa Red Star Belgrade Mserbia Strahinja Stojkovic aliye na umri wa miaka 17. (Football Insider)

Arsenal wamefanya mazungumzo na mawakala wa shambuliaji wa Sporting Geovany Quenda, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 pia akiwaniwa na na Manchester United, Manchester City na Liverpool. (Team Talk)

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 36, yuko tayari kupunguziwa mshahara ili kusalia Barcelona na kiwango chake kizuri kimeifanya klabu hiyo ya Catalan kupoza hamu ya kumnunua mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland, 24, kutoka Norway. (Sport - kwa Kihispania)

AC Milan wako tayari kuongeza mara mbili mishahara ya kiungo wa Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, asinyakuliwe na Manchester City na Tottenham. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Manchester City wanamfuatilia kiungo wa kati wa Inter Milan Hakan Calhanoglu, 30, ingawa Bayern Munich wako katika nafasi nzuri ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki. (Caughtoffside)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta atakuwa na uamuzi ni nani kuchukua nafasi ya Edu kama mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo baada ya Mbrazil huyo kuamua kuachana na The Gunners. (Times - usajili unahitajika)

West Ham wanaamini kwamba mkurugenzi wa ufundi Tim Steidten anaweza kuzingatiwa na Arsenal kama mbadala wa Edu. (Telegraph - usajili unahitajika)

Beki wa Tottenham Cristian Romero huenda akahamia Real Madrid msimu huu wa joto ikiwa klabu hiyo ya La Liga itaimarisha mpango wa kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 26. (GiveMeSport - usajili unahitajika)

Paris St-Germain wako tayari wamefutilia mbali uhamisho wa mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 26, licha ya ufungaji mabao wake mahiri katika klabu ya Sporting. (Le Parisien - kwa Kifaransa)

Arsenal bado wanavutiwa na mshambuliaji wa RB Leipzig raia wa Slovenia Benjamin Sesko, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akiwa na kipengele cha kumnunua cha £55m katika mkataba wake. (Mail - usajili unahitajika)

Mkufunzi wa Wolves Gary O'Neil huenda akafutwa kazi ikiwa timu yake haitaifunga Southampton katika mechi ya Ligi ya Premia wikendi hii. (Telegraph - usajili unahitajika)

Paris St-Germain wako tayari kumruhusu mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 25, kuondoka mwezi Januari huku klabu za Ligi ya Premia na Bundesliga zikiwa tayari kumnunua. (RMC Sport - kwa Kifaransa)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
1h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
3h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
4h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
4h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
5h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
8h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
10h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
11h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
11h ago
READ MORE β†’